Song Lyrics
[Chorus]
Nimeonja pendo Lako
Nami najua We U mwema
Njia Zako nimezitambua
Kweli hakuna kama Wewe
[Verse 1]
Kila wakati nitakuhimidi Bwana
Sifa Zako zi kinywani daima
Kwako wewe, nafsi yangu itajisifu
Wasikie wafurahie wanyenyekevu
Nilikutafuta ukanijibu
Ukaniponya kwa zangu zote masaibu
Usifiwe, uabudiwe Bwana
Hakuna kama Wewe
[Verse 2]
Nikiugua, Wewe waniponya
Nikianguka waniinua
Wewe ni ngao yangu pande zote
Sina hofu sibabaiki kamwe
Kwa sauti mimi nitaimba
Mataifa yote yasikie
Kuwa wewe pekee
Ndiye Mkuu
Comments / Requests
Album Artwork

Album Tracks
Other Useful Links: