Song Lyrics

"Natamani Nikuone"

by Laura Karwirwa
Album: Natamani Nikuone

Mengi nimeshasikia, uliyoyatenda
Mengi hata nami pia, naweza shuhudia
Katika siku zangu za giza, wewe umenituliza
Nimepenya kwenye giza, umenimulikia njia
[Prechorus]
Nikusujudie, nikuinamie, niseme nawe
Niushike mkono wako ewe oh , nitembee nawe
[Chorus]
Natamani nikuone.. Eeh
Ndiyo tamaa ya moyo wangu
Na nafsi yangu (Repeat 2x)
Umekuwa mwemaaa (Repeat 4x)
Nitakuwa nimetayarisha sadaka nikupe
Na sauti nimenyorosha na malaika niimbe
Sadaka za sifa
Naomba pokea
Sauti napaza, napaza
Naomba sikia
[Bridge]
Natambua mimi dhaifu
Kama Musa ninavua viatu vyangu
Nikaribie utakatifu wako
Nimeoshwa na hiyo damu


Music Video
Comments / Requests
Album Artwork
Other Useful Links: